BAJETI ZA MIUNDOMBINU YA ELIMU ZITENGWE KUJIANDAA NA MAPOKEZI YA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA 2028 - PROF. SHEMDOE

BAJETI ZA MIUNDOMBINU YA ELIMU ZITENGWE KUJIANDAA NA MAPOKEZI YA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA 2028 - PROF. SHEMDOE
Na OWM – TAMISEMI, Bagamoyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa kuhakikisha wanawasimamia Wakurugezi wa Halmashauri wakati wanapoandaa bajeti za Mwaka wa Fedha 2026/27 kuweka vifungu vya kugharamia maboresho ya miundombinu ya elimu, ili kujiaanda na mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2028 ambapo kwa mujibu wa mtaala mpya watapokelewa wanafunzi waliohitimu darasa la sita na la saba. Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo leo, akiwa katika kikao kazi cha kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Halmashauri ya Mji Bagamoyo, mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya mendeleo katika halmashauri hiyo ya mji.  “Mwaka 2028 kutokana na mtaala mpya watakaohitimu darasa la sita na la saba watajiunga na kidato cha kwanza, hivyo yatengwe mafungu kwenye bajeti mtakazoandaa ili kusiwe na maandalizi ya zimamoto tunapojianda kupokea wanafunzi hao,” a…