ZIARA ZA MAJIMBO 50 ZINALENGA KUIMARISHA UHAI WA CCM - NDG. ABDI:
ZIARA ZA MAJIMBO 50 ZINALENGA KUIMARISHA UHAI WA CCM - NDG. ABDI:
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, amesema ziara zake katika majimbo 50 na matawi yake zinalenga kuimarisha uhai wa Chama, kusikiliza changamoto zinazowakabili wanachama na kuhamasisha utekelezaji wa Ilani ya CCM. Ndg. Abdi ameyasema hayo leo, Septemba 13, 2026, wakati akiendelea na ziara za kukagua uhai wa CCM katika Tawi la Pita na Zako, Jimbo la Kijini, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Amesema ziara hizo pia zinalenga kuhamasisha viongozi na wanachama wa CCM kuunga mkono juhudi zinazofanywa na viongozi wakuu wa Serikali katika kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi. Amesema CCM itaendelea kuisimamia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha inatekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama, ikiwemo kuweka mazingira bora kwa wananchi, hususan wakulima wa mwani, kupata masoko ya uhakika yatakayowawezesha kuongeza kipato na kuboresha maisha yao. Kwa upande wake, Katibu wa Idara ya Organisation wa CCM Zanzibar, Ndg. Omar Ibrahim Kilupi, amewataka wana…