WMA YAIMARISHA UWAJIBIKAJI NA WELEDI WA WATUMISHI GEITA
WMA YAIMARISHA UWAJIBIKAJI NA WELEDI WA WATUMISHI GEITA
Na. WMA – Geita 2 Septemba, 2026 📍 “Vipimo Sahihi, Huduma Bora, Haki kwa Wote” Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Christopher Mwakibinga, amefanya kikao kazi na watumishi wa WMA Mkoa wa Geita, akisisitiza umuhimu wa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu, pamoja na kuongeza uwajibikaji na weledi katika utekelezaji wa majukumu. Katika kikao hicho, Bw. Mwakibinga amewataka watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu huku wakiongozwa na busara. Aidha, amewataka Maafisa Vipimo kuzingatia miongozo ya kazi (Standard Operating Procedures – SOPs) katika utekelezaji wa majukumu yao. Amesisitiza pia umuhimu wa nidhamu kazini, ikiwemo kuwahi kazini na kuzingatia taratibu za kupata ruhusa ya kimaandishi wakati wa kusafiri nje ya kituo cha kazi. Vilevile, amewataka watumishi kuheshimu viongozi wao na kutunza mali na vifaa vya Wakala, hususan magari, ili viendelee kutumika kwa ufanisi katika kutekeleza majukumu ya WMA. Kwa upande mwingine, Bw. Mwak…