WAZIRI SANGU ASISITIZA UFUATILIAJI NA TATHMINI KATIKA KUFANYA MAAMUZI BORA
WAZIRI SANGU ASISITIZA UFUATILIAJI NA TATHMINI KATIKA KUFANYA MAAMUZI BORA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, akizungumza katika Mkutano wa Kwanza wa Wakurugenzi na Wasimamizi wa Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini uliofanyika leo Septemba 21, 2026, jijini Arusha. *************** Na OWM (KAM), Arusha WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema Vitengo vya ufuatiliaji na tathmini vinawajibu wa kuisaidia serikali kufanya maamuzi sahihi, kuboresha utekelezaji wa mipango na kuhakikisha matumizi ya rasilimali za umma yanaleta matokeo chanya kwa wananchi. Akifungua Mkutano wa Kwanza wa Wakurugenzi na Wasimamizi wa Vitengo hivyo leo Septemba 21, 2026, jijini Arusha, Mhe. Sangu amesema wataalamu wa vitengo hivyo wana jukumu la kuhakikisha mipango ya Serikali inatafsiriwa kuwa matokeo halisi yanayoboresha maisha ya wananchi. “Wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini, ninyi ndiyo macho, pua na masikio mnaojenga mfumo wa Serikali wa kujua kama mipango tunayoiweka kwenye karatasi inabadili…