Waziri Kombo Aagana na Balozi wa DRC Nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amekutana na kuagana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mheshimiwa Jean Pierre Massala, ambaye amehitimisha muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Mhe. Kombo alikutana na Balozi huyo Septemba 4, 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Waziri Kombo alimpongeza Balozi Massala kwa mchango wake katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa pande mbili kati ya Tanzania na DRC, hususan katika maeneo ya maendeleo, biashara na uwekezaji. Waziri Kombo alisema Tanzania imeazimia kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati na DRC katika sekta mbalimbali, zikiwemo uchukuzi, madini, mafuta na gesi, ulinzi na usalama, pamoja na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya pamoja yenye manufaa kwa wananchi wa nchi hizo mbili. Miongoni mwa miradi ya kipaumbele ni ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), inayolenga kuunganisha Tanzania na DRC kupitia …