WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUENDELEA KUWAFUTILIA WATOTO WAO BAADA YA KUHITIMU

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUENDELEA KUWAFUTILIA WATOTO WAO BAADA YA KUHITIMU
Askofu mkuu mwangalizi wa makanisa ya Wabatisti Tanzania,Askofu Anold Manase wakati akizungumza katika mahafali hayo Na Happy Lazaro, Arusha Wazazi pamoja na walezi wametakiwa kuendelea kuwafuatilia watoto wao kwani kuhitimu darasa la saba sio kuhitimu maisha wala malezi kwani bado wana nafasi kubwa ya kuwafuatilia mpaka watakapofikia hatua ya wao kujitegemea. Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Askofu mkuu mwangalizi wa makanisa ya Wabatisti Tanzania,Askofu Anold Manase wakati akizungumza katika mahafali ya ya darasa la saba katika shule ya mchepuo wa kiingireza ya Maromboso Baptist iliyopo kata ya Ngarenaro jijini Arusha . Askofu Manase amesema kuwa,wazazi na walezi bado wana nguvu ya kuwekeza kwa watoto wao kwa kupewa malezi ya kijimudu wenyewe ili waweze kujitegemea kwa maisha yao ya baadaye. “Nawaombeni sana wazazi na walezi muendelee kuwafuatilia watoto wenu kwa karibu kwani wanahitaji uangalizi mkubwa ili waweze kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kujiepusha na makundi yasiy…