WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO KUATHIRIKA NA TATIZO LA MISULI YA MOYO (DILATED CARDIOMYOPATHY – DCM)
Na Mwandishi Maalumu , Dar es Salaam. Watoto wenye umri chini ya miaka mitano uathirika zaidi na ugonjwa wa misuli ya moyo unaojulikana kitaalamu kama Dilated Cardiomyopathy (DCM), huku historia ya maambukizi ya misuli ya moyo (myocarditis) ikitajwa kuwa sababu inayoongoza miongoni mwa sababu zilizobainika. Hayo yamebainishwa katika utafiti uliofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Januari 2021 hadi Desemba 2025 uliangalia taarifa za watoto waliolazwa JKCI wakiwa na ugonjwa huo kwa lengo la kuchambua sifa za ugonjwa pamoja na matokeo ya matibabu yake. Kwa mujibu wa utafiti huo, jumla ya watoto 3,330 waliolazwa JKCI katika kipindi hicho watoto 45 sawa na asilimia 1.4, waligundulika kuwa na tatizo la DCM, Hata hivyo watoto 10 waliondolewa katika utafiti kutokana na kutokamilika kwa taarifa zao za kitabibu hivyo utafiti kujumuisha watoto 35. Akizungumzia utafiti huo Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto aliyefanya utafiti hu…