WANANCHI ZAIDI YA 3,800 WANUFAIKA NA KAMBI YA MATIBABU NA UPASUAJI WA MACHO ILIYOENDESHWA NA MUHIMBILI ZANZIBAR
WANANCHI ZAIDI YA 3,800 WANUFAIKA NA KAMBI YA MATIBABU NA UPASUAJI WA MACHO ILIYOENDESHWA NA MUHIMBILI ZANZIBAR
Jumla ya wananchi 3,879 wamenufaika na Kambi Maalum ya Matibabu na Upasuaji wa Macho iliyoendeshwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Qatar Charity, iliyohitimishwa leo Septemba 4, 2026 katika viwanja vya Kituo cha Afya Sebuleni, Mkoa wa Mjini Magharibi. Akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mhe. Mohammed Ali Abdalla, amesema huduma hiyo imeleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa matibabu ya macho Zanzibar kwa kuwafikia wananchi moja kwa moja katika maeneo yao na kueleza kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuthamini ushirikiano na Muhimbili na Qatar Charity katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi. “Leo tunashuhudia maelfu ya wananchi wakirejeshewa matumaini ya kuona. Ushirikiano huu umeonesha kuwa tukifanya kazi pamoja tunaweza kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi na kupunguza adha ya kusafiri kutafuta matibabu." amesema Mhe. Abdalla Kwa up…