WAKUU WA TAASISI ZA MUUNGANO WATAKIWA KUIMARISHA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI

WAKUU WA TAASISI ZA MUUNGANO WATAKIWA KUIMARISHA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI
ZANZIBAR, Septemba 19, 2026 — Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, amewataka Wakuu wa Taasisi za Muungano kuimarisha ushirikiano na utekelezaji wa majukumu yao ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora bila kujali wanaishi upande gani wa Muungano. Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo leo Septemba 19, 2026, wakati akifungua kikao maalum cha Wakuu wa Taasisi za Muungano kilichofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Airport, Zanzibar. Kikao hicho kimejadili masuala mbalimbali yanayohusu uratibu na utekelezaji wa masuala ya Muungano, huku Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt. Erasmus Kipesha, akiwa miongoni mwa Wakuu wa Taasisi walioshiriki. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Ndejembi amesema kila Mkuu wa Taasisi anapaswa kuwa na uelewa wa maana ya Muungano pamoja na dhana na majukumu yanayohusiana na masuala ya Muungano. Amesema kila Mtanzania anahitaji huduma bora na kwamba jukumu la kuhakikisha huduma hizo zinapatikana ni la Taasisi…