WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA MBEGU BORA KUKABILIANA NA UKAME

WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA MBEGU BORA KUKABILIANA NA UKAME
Ofisa Masoko wa Kijani Consultant, Franswer Lawrence,  leo akitoa elimu kwa wananchi kwenye Maonesho ya 21 ya Biashara ya Afrika Mashariki (MEATF 2026), yanayofanyika katika Uwanja wa Furahisha, Wilaya ya Ilemela, Mwanza.Picha zote na Baltazar Mashaka ……. Na BALTAZAR MASHAKA, MWANZA WAKULIMA wa mahindi na mpunga wametakiwa kutumia mbegu bora zilizoboreshwa zinazostahimili ukame, magonjwa na wadudu waharibifu ili kuongeza tija na mavuno katika kilimo, hasa wakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Ushauri huo umetolewa leo na Ofisa Masoko wa Kijani Consultant, Franswer Lawrence, wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Maonesho ya 21 ya Biashara ya Afrika Mashariki (MEATF 2026), yanayofanyika katika Uwanja wa Furahisha, Wilaya ya Ilemela, Mwanza. Lawrence alisema uchaguzi wa mbegu bora kulingana na mazingira ya eneo la mkulima ni hatua muhimu ya kuongeza uzalishaji, kwani baadhi ya mbegu zimeboreshwa kuwa na uwezo wa kustahimili ukame na changamoto nyingine zinazoweza kupunguz…