WAKULIMA BABATI WANUFAIKA NA PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI (AFDP)
WAKULIMA BABATI WANUFAIKA NA PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI (AFDP)
Na; Mwandishi wetu – Babati Wakulima wa vijiji vya Endakiso na Orng'adida vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wameeleza kunufaika na Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwa kushirikina na Serikali na kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, na wenye Ulemavu. Kwa nyakati Tofauti wakulima kutoka vijiji hivyo wameyasema hayo tarehe 4 Septemba wakati wa ziara ya timu kutoka IFAD inayotathimini maendeleo ya utekelezaji Programu ya muda wa kati (MTR). Wakulima hao waliweka bayana kuwa, Programu hiyo imeweza kuwaletea teknolojia ya kisasa ya Kilimo Mseto kwa kutumia Mbegu himilivu zinazoweza kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi. Akizungumza wakati wa Ziara hiyo Bw. Ramadhani Iddi Mfumbilo mkulima kutoka katika kijiji cha Mkombozi Kata ya Endasiko alisema, kupitia Programu hii wakulima wameweza kupata mbegu za mahindi aina ya situka na mbegu za lishe …