WADAU WA KILIMO-MISITU WAANZISHA JUKWAA LA KITAIFA (TASP)
WADAU WA KILIMO-MISITU WAANZISHA JUKWAA LA KITAIFA (TASP)
Wadau wa kilimo-misitu nchini Tanzania wameanzisha jukwaa maalum (TASP), litakalowaunganisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, taarifa na ubunifu, pamoja na kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza kilimo-misitu na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Akifungua jukwaa hilo Septemba 10, 2026 jijini Dodoma, Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Nickson Kimaro, amesema kilimo-misitu ni agenda mtambuka inayohitaji ushirikiano wa Serikali, wakulima, taasisi za utafiti, sekta binafsi, asasi za kiraia, taasisi za fedha na washirika wa maendeleo. Amesema TASP inapaswa kuwa mfumo endelevu wa uratibu utakaowezesha wadau kuoanisha jitihada zao, kubaini mapungufu na kutumia rasilimali kwa ufanisi, huku kilimo-misitu kikiwa na manufaa ya kiuchumi, kijamii na kimazingira. Mkurugenzi Mtendaji wa Civic Social Protection Foundation (CPS), Nemence Iriya, amesema jukwaa hilo litatoa nafasi kwa wadau kukutana na kujadili sera, mikakati, sheria na taratibu zinazohusu k…