VYOMBO VYA HABARI NCHINI VYASIMAMA KIDETE KUSAKA SULUHU YA TAARIFA POTOFU NA MATAMSHI YA CHUKI
VYOMBO VYA HABARI NCHINI VYASIMAMA KIDETE KUSAKA SULUHU YA TAARIFA POTOFU NA MATAMSHI YA CHUKI
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu na matamshi ya chuki (hate speech), jijini Arusha. *** Waandishi wa habari, wahariri, na wataalamu wa masoko kutoka taasisi kumi za habari nchini Tanzania wamejengewa uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto ya taarifa potofu, upotoshaji, na matamshi ya chuki kupitia mafunzo maalum ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji yanayofanyika kwa siku tatu mfululizo jijini Arusha kuanzia Septemba 9 hadi 11, 2026. Mafunzo haya ya kimkakati yanayoendeshwa na Shirika la International Media Support (IMS) kwa kushirikiana na Kampuni ya Teknolojia na Habari ya Nukta Africa, Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), na JamiiAfrica, yanalenga kuwezesha vyombo vya habari kuandaa mawazo na suluhu zinazozingatia mahitaji, uzoefu, na tabia halisi za wananchi wanaotumia taarif…