VIKUNDI 203 VYASAJILIWA NZEGA DC
Na Mwandishi wetu, Nzega HALMASHAURI ya Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora, imesajili vikundi 203 vikijumuisha wazee 11, wanawake 108, vijana 79 na watu wenye ulemavu watano. Afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, AnnaMary Galibona ameeleza hayo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2026 Wazo Michael Mwang’onda akisoma taarifa ya usajili na ushiriki wa makundi maalumu kwenye mfumo wa ununuzi wa umma (PPRA). Galibona ameeleza kwamba hadi kufikia Septemba mwaka 2026 vikundi hivyo vimeshasajiliwa na Halmashauri hiyo na wana mikakati ya kuongeza zabuni kwa makundi maalum. Amesema kwa mwaka 2026 vikundi tisa vimetunukiwa zabuni mbalimbali zenye thamani ya shilingi 76,000,000 ambapo vikundi viwili vipo katika hatua ya utekelezaji wa mikataba ya thamani ya shilingi 13,000,000 na vikundi saba vipo hatua ya kusaini mikataba yenye thamani ya 63,000,000 iliyotolewa na TARURA. Amesema hiyo ni miongoni mwa Halmashauri zinazotekeleza sheria ya ununuzi wa umma ya mwa…