VIJANA  WATAKIWA KUTUMIA MAJUKWAA YA MAFUNZO KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la  Smarticents , Klein  August akizungumza kwenye jukwaa hilo jijini Arusha …………… Na Happy Lazaro, Arusha  Vijana  nchini  wametakiwa kutumia majukwaa ya mafunzo, semina na mijadala mbalimbali kama fursa ya kujifunza, kujenga mitandao na kutafuta njia mpya za kujikwamua kiuchumi. Hayo yamesemwa jijiji Arusha na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la  Smarticents , Klein  August  wakati akizungumza katika Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Arusha, lililowakutanisha viongozi wa Serikali, mashirika ya kiraia na wadau wa maendeleo kujadili nafasi ya NGOs katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Klein amesema shirika hilo  limejikita katika kutoa elimu ya fedha kwa vijana pamoja na makundi maalumu  katika jamii, huku ikiendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kusimamia shughuli zao na kuongeza kipato. Amesema kuwa, ushiriki wake katika tukio hilo umempa nafasi ya…