VIJANA WATAKIWA KUANDALIWA UONGOZI TANGU WAKIWA WADOGO
VIJANA WATAKIWA KUANDALIWA UONGOZI TANGU WAKIWA WADOGO
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM VIJANA nchini wametakiwa kupewa mafunzo ya uongozi tangu wakiwa katika umri mdogo ili kuwaandaa kuwa viongozi wenye maadili, uwajibikaji na uwezo wa kuongoza katika nyanja mbalimbali, hatua inayolenga kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Wito huo umetolewa wakati Shirika la African Leadership Initiatives for Impact (ALII), kwa kushirikiana na HakiElimu na kwa uwezeshaji wa Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, Norwegian Church Aid na UTT AMIS, likizindua awamu ya pili ya Programu ya Tanzania NextGen Leaders Fellowship (TNLF Cohort 2). Programu hiyo inalenga kuwaandaa vijana kuwa viongozi wenye maono, maadili na uwezo wa kuchangia katika maendeleo ya taifa. Uzinduzi wa programu hiyo ulifanyika leo katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ukihudhuriwa na vijana 100 waliochaguliwa kushiriki katika kundi hilo, pamoja na viongozi, wataalamu, wadau wa maendeleo na wawakilishi wa taasisi mbalimbali. Akizungumza katika hafla hiyo, …