VIJANA WAHIMIZWA KUCHUKUA HATUA LEO, ELIMU YAO IWANUFAISHE JAMII
VIJANA WAHIMIZWA KUCHUKUA HATUA LEO, ELIMU YAO IWANUFAISHE JAMII Mkurugenzi wa shule za Intels pre ,primary na sekondari ,Alexander Samson akizungumza kwenye mahafali hayo jijini Arus Mwandishi mwandamizi wa vitabu mbalimbali ,Joramu Nkumbi akizungumza katika mahafali hayo jijini Arusha Happy Lazaro, Arusha. Arusha .VIJANA nchini wametakiwa kuacha mtazamo wa kusubiri kuwa “Taifa la kesho” na badala yake kuchukua hatua sasa kwa kutumia elimu, vipaji, maarifa na uwezo walionao katika kuleta mabadiliko katika familia, jamii na taifa kwa ujumla. Hayo yamesemwa na mgenirasmi ambaye ni ,Mwandishi mwandamizi wa vitabu mbalimbali ,Joramu Nkumbi katika mahafali ya shule za Intels ambapo kwa upande wa kidato cha 4 ni mahafali ya 8 na mahafali ya 20 darasa la saba . Nkumbi amesema vijana ni sehemu muhimu ya Taifa la leo na kesho, hivyo wanapaswa kujiamini, kuthubutu kufanya mambo makubwa, kuzungumza na kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili badala ya kusubiri nafasi kutoka kwa wengine. “Vijana ni taifa la leo, lakini pia ni taifa la kesho. Vijana ni vio…