VETA, VAN MO ZASAINI MAKUBALIANO KUENDELEZA UJUZI NA AJIRA KWA VIJANA

VETA, VAN MO ZASAINI MAKUBALIANO KUENDELEZA UJUZI NA AJIRA KWA VIJANA
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Kampuni ya Van Mo zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) yenye lengo la kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza ujuzi kwa vijana na kuwaandaa kupata ajira kulingana na mahitaji ya soko. Hati hiyo imesainiwa leo, Septemba 4, 2026, jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, pamoja na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Van Mo, Fathi Ahmed. Ushirikiano huo unalenga kuhakikisha mafunzo ya ufundi stadi yanaendana na mahitaji ya sekta ya viwanda na biashara, huku wahitimu wakijengewa umahiri, ubunifu, tija, maadili na uelewa wa usalama kazini, Van Mo pia itatoa fursa za mafunzo kwa vitendo na ajira kwa wahitimu wenye sifa zinazokidhi mahitaji yake. Maeneo yatakayohusika katika makubaliano hayo ni pamoja na udereva wa magari makubwa, usimamizi wa vyombo vya usafiri, uchukuzi na uhifadhi wa mizigo, usimamizi wa mnyororo wa ugavi, ukaguzi na ukarabati wa magari pamoja na mifumo ya umeme na elektroniki ya magari. Maeneo mengine ni uendesh…