UWEKEZAJI UNAOFANYWA NA SERIKALI KATIKA AFYA YA MSINGI NDIO MSINGI WA AFYA KWA WOTE – PROF .SHEMDOE

UWEKEZAJI UNAOFANYWA NA SERIKALI KATIKA AFYA YA MSINGI NDIO MSINGI WA AFYA KWA WOTE – PROF .SHEMDOE
OWM -TAMISEMI Arusha   Serikali imesisitiza kuwa inaendea kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa vifaa tiba katika ngazi ya Afya ya Msingi, ikiwa ni hatua muhimu ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya kwa wakati. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Silas Shemdoe (Mb.), wakati akitoa salamu za ofisi yake katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Afya ya Msingi unaofanyika Arusha jijini Arusha katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC). Prof. Shemdoe amesema takwimu za mwaka 2025 zinaonesha umuhimu mkubwa wa vituo vya Afya ya Msingi, ambapo kati ya wajawazito milioni 2.09 waliojifungulia katika vituo vya afya vya umma, milioni 2 sawa na asilimia 95.6 walipata huduma katika ngazi hiyo. Aidha, amefafanua kuwa kati ya mahudhurio milioni 32.3 ya wagonjwa wa nje katika vituo vya umma, milioni 27.8 sawa na asilimia 86 yalifanyika katika vituo vya Afya ya Msingi. Amesema kati ya vituo 8,288 vya afya vya Serikali nchin…