UJENZI SPORTS CLUB YATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM DODOMA

UJENZI SPORTS CLUB YATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM DODOMA
Timu ya Ujenzi Sports Club imeendelea kuunga mkono juhudi za kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlezi jijini Dodoma. Msaada huo umetolewa Jumatano, Septemba 2, 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Ujenzi Sports Club kuunga mkono kazi inayofanywa na shule hiyo katika kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na wanafunzi wengine kupata mazingira bora ya kujifunzia. Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na madaftari, vyombo vya kulia chakula, vifaa vya usafi, sabuni, ndoo pamoja na fedha kwa ajili ya ununuzi wa mipira ya michezo. Akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Ujenzi Sports Club, Arch. Ibrahim Chatila, amesema klabu hiyo inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na walimu katika kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kutimiza ndoto zao kielimu na katika maisha kwa ujumla. Amesema msaada huo ni sehemu ya jitihada za Ujenzi Sports Club kuunga mkono juhudi zinazofanywa na shule hiyo, huku akiahidi kuwa…