UFUATILIAJI NA TATHMINI KISISUBIRIE MWISHO WA MWAKA KUTAMBUA MALENGO HAYAJAFIKIWA
UFUATILIAJI NA TATHMINI KISISUBIRIE MWISHO WA MWAKA KUTAMBUA MALENGO HAYAJAFIKIWA
Na Vero Ignatus – Michuzi TV, Arusha Kongamano la Tano la Taifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linalofanyika jijini Arusha kuanzia Septemba 22 hadi 26, 2026, limeendelea kupata mafanikio makubwa baada ya kuweka rekodi ya kukusanya jumla ya washiriki 1,664 kutoka ndani na nje ya nchi Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo Hoteli ya Ngurdoto Wilayani Arumeru mkoani Arusha,Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Daniel Sillo akimuwakilisha Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, amezitaka taasisi za umma kutumia mfumo wa ufuatiliaji na tathmini kama kifaa cha kutoa tahadhari ya awali badala ya kusubiri hadi mwisho wa mwaka. "Ufuatiliaji na tathmini ni chombo muhimu cha usimamizi katika taasisi. Msisubiri mwisho wa mwaka ndipo mtambue kwamba shabaha hazijafikiwa," amesema Mhe. Sillo. Amesema viongozi na watendaji wa Serikali wanapaswa kusoma na kujadili taarifa hizo kwenye vikao vya menejimenti ili kuchukua hatua za haraka pale changamoto zinapob…