TMDA, POLISI KUIMARISHA MBINU ZA KUDHIBITI DAWA BANDIA NCHINI

TMDA, POLISI KUIMARISHA MBINU ZA KUDHIBITI DAWA BANDIA NCHINI
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam  Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imeanza kuimarisha mbinu za kudhibiti uingizaji, usambazaji na matumizi ya dawa bandia na bidhaa nyingine zisizokidhi viwango nchini. Akizungumza katika kikao kazi kati ya TMDA na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TMDA, Adam Fimbo, amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanatumia dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa za tumbaku zenye ubora, usalama na ufanisi. Amesema TMDA ina jukumu la kudhibiti bidhaa hizo kuanzia hatua ya usajili, uingizaji nchini, usambazaji hadi matumizi, ili kuhakikisha zinakidhi viwango vinavyotakiwa. “Majukumu yetu makubwa ni kuhakikisha bidhaa hizo ni bora, salama na zina ufanisi kwa matumizi ya binadamu na mifugo,” amesema. Amesema kabla ya bidhaa kuingia nchini, lazima zisajiliwe na mamlaka hiyo baada ya kuthibitishwa kupitia tafiti na uchunguzi wa kitaalamu unaoonyesha kuwa zina ubora, usalama na ufanisi unaokuba…