TIRA YASHAURI KAMPUNI ZA BIMA ZITOE MAJIBU KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANANCHI

TIRA YASHAURI KAMPUNI ZA BIMA ZITOE MAJIBU KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANANCHI
-Yazindua bidhaa tatu za Jubilee Life Insurance ambazo ni Fanaka Plus, Smart Education Insurance Plan na Akiba Flex Plan Na Said Mwishehe, Michuzi TV MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imezitaka kampuni za bima kubuni bidhaa zinazotoa majibu ya vitendo kwa changamoto zinazowakabili wananchi, ikisema ubora wa bidhaa za bima haupaswi kupimwa kwa idadi ya watu waliojiunga pekee. Kamishna wa Bima, Dk.Baghayo Saqware amesema kampuni zinazolenga kuongeza ujumuishi wa kifedha zinapaswa kwanza kuelewa mazingira wanamoishi Watanzania na changamoto zinazowakabili kabla ya kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji yao. Dk.Saqware ametoa kauli hiyo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Uzingatiaji wa Sheria na Kanuni wa TIRA, Bw Alex Rock wakati wa uzinduzi wa bidhaa tatu mpya za bima ya maisha za Jubilee Life Insurance Tanzania uliofanyika leo Septemba 3,2026 jijini Dar es Salaam. “Mwito wangu kwa Jubilee Life Insurance na kampuni nyingine za bima ni kuendelea kubuni bidhaa zina…