TEKNOLOJIA ISIWE SABABU YA WAANDISHI WA HABARI KUKIUKA MAADILI
TEKNOLOJIA ISIWE SABABU YA WAANDISHI WA HABARI KUKIUKA MAADILI
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kutoruhusu maendeleo ya teknolojia kuathiri uzingatiaji wa maadili na misingi ya taaluma wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa Habari wa EFM na TVE, yaliyofanyika Septemba 9 na 10, 2026 katika Ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam. “Mkiwa Waandishi wa Habari, mna wajibu wa kuhakikisha mnasimamia misingi ya taaluma kwa kuzingatia sheria, kuepuka kutoa taarifa za uongo na kujiepusha na makosa ya jinai,” amesema Wakili Kipangula. Kwa upande wake, Msaidizi wa Mkuu wa Vipindi wa EFM, Bw. Evalist Razeck, amewasihi wamiliki wa vyombo vya habari kuwapa Waandishi wa Habari fursa ya kushiriki mafunzo ya mara kwa mara ili kujikumbusha misingi muhimu ya taaluma na kuwawezesha kukusanya na kutoa taarifa zenye tija kwa jamii wanayoihudumia. Naye Mtangazaji wa EFM, Bi. Fatuma Muhidini Likwata, …