TCRS NA HALMASHAURI YA KISHAPU WAENDELEZA UTOAJI ELIMU DHIDI YA EL NINO

TCRS NA HALMASHAURI YA KISHAPU WAENDELEZA UTOAJI ELIMU DHIDI YA EL NINO
Na Sumai Salum-Kishapu Shirika la Tanganyika Christian Refugee Services (TCRS) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga, ikiwemo mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño, katika Kijiji cha Ilebelebe, Kata ya Itilima wilayani humo. Elimu hiyo imetolewa Agosti 24, 2026 katika mkutano wa hadhara na wananchi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa programu inayolenga kuimarisha uelewa na uwezo wa jamii kuchukua tahadhari na kukabiliana na majanga kabla, wakati na baada ya kutokea. Afisa Miradi wa TCRS Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Sanyenge, amesema miongoni mwa miradi inayotekelezwa na shirika hilo ni pamoja na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira, udhibiti wa taka na namna jamii inavyoweza kujiandaa na kukabiliana na athari za mvua kubwa za El Niño. Amesema programu hiyo inatekelezwa katika Kata 10 zilizobainishwa kuwa katika hatari ya kukumbwa na mafuriko, ambazo n…