TBS YAIBUKA MSHINDI WA PILI KATIKA MAONESHO YA 21 YA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI (MEATF)

TBS YAIBUKA MSHINDI WA PILI KATIKA MAONESHO YA 21 YA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI (MEATF)
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeibuka mshindi wa pili katika kundi la Taasisi za Udhibiti wakati wa Maonesho ya 21 ya Biashara Afrika Mashariki (MEATF), yanayofanyika katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza. Ushindi huo unaonesha namna TBS inavyoendelea kutekeleza jukumu lake la kuhakikisha bidhaa na huduma zinazotolewa nchini zinakidhi matakwa ya viwango, pamoja na kujenga uelewa wa matumizi ya viwango miongoni mwa wazalishaji, wafanyabiashara na wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa Mashariki, Happy Brown, amesema ushindi huo unaonesha dhamira ya TBS ya kuendelea kuwafikia wananchi na wadau mbalimbali kupitia utoaji wa elimu kuhusu viwango, ubora na usalama wa bidhaa. Amesema ushiriki wa TBS katika maonesho hayo umeendelea kuwa fursa muhimu ya kuwahudumia wananchi, hasa wajasiriamali na wafanyabiashara, kwa kuwaelimisha kuhusu viwango vinavyohitajika katika shughuli zao na kuwawezesha kupata huduma mbalimbali za TBS. “Ushindi huu unaonesha dh…