TARURA YATUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA KUCHUNGUZA UDONGO KABLA YA UJENZI WA MIUNDOMBINU

TARURA YATUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA KUCHUNGUZA UDONGO KABLA YA UJENZI WA MIUNDOMBINU
Na mwandishi wetu, Dodoma ‎Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeanza kutumia teknolojia ya kisasa kufanya uchunguzi wa kina wa udongo kabla ya ujenzi wa miradi ya barabara, madaraja na miundombinu mingine hatua inayolenga kuongeza usalama, ubora na uimara wa miradi ili iweze kudumu kwa muda mrefu ikiwemo kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. ‎Hatua hiyo inawawezesha wataalamu kupata taarifa za kina kuhusu tabaka za udongo na miamba zilizopo chini ya ardhi hivyo kusaidia kubaini aina ya msingi na mbinu za ujenzi zinazofaa kulingana na mazingira ya eneo husika. ‎Akizungumza jijini Dodoma wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika maabara za TARURA, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tafiti na Udhibiti Ubora wa Wakala huo, Mhandisi Vincent Lwanda amesema uchunguzi wa udongo ni miongoni mwa hatua muhimu katika kuhakikisha miundombinu inayojengwa inakuwa salama, imara na yenye uwezo wa kudumu kwa muda mrefu. ‎Amesema TARURA imekuwa ikifanya tafiti kuhusu udongo pamoja na …