TANZANIA YAWAALIKA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA SEKTA YA MADINI

TANZANIA YAWAALIKA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA SEKTA YA MADINI
 Perth, Australia  Tanzania imeendelea na mkakati wa kuwaalika wawekezaji wa kimataifa kutumia fursa zilizopo katika Sekta ya Madini nchini, kwa kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuongeza taarifa za kijiolojia na kuendeleza miradi mikubwa ya madini yenye uwezo wa kuongeza thamani ya uchumi wa taifa.  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, leo Septemba 03, 2026, mjini Perth, Australia wakati akizungumza katika Mkutano wa 24 wa Africa Down Under 2026 ambapo amesema Tanzania imefika kwenye jukwaa hilo ikiwa na ujumbe ulio wazi. “Tuna madini. Tunawekeza katika maarifa na uendelezaji wa ujuzi; tunaboresha mazingira ya uwekezaji; na tuko tayari kushirikiana na wawekezaji.” amesema Kiruswa. Amesema Sekta ya Madini imeendelea kuwa injini muhimu ya uchumi wa Tanzania, ambapo mchango wake katika Pato la Taifa umefikia asilimia 10.3 mwaka 2025, huku ikichangia takribani asilimia 53 ya thamani ya mauzo yote ya nje ya nchi. Aidha, uzalishaji wa dhahab…