TANZANIA, MISRI ZAAZIMIA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA NA KIUCHUMI
TANZANIA, MISRI ZAAZIMIA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA NA KIUCHUMI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amesema Tanzania na Misri zimedhamiria kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa nchi hizo katika biashara, uwekezaji, miundombinu, elimu, afya na masuala ya kimataifa. Waziri Kombo amesema hayo katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia pia Ushirikiano wa Kimataifa na masuala ya Wamisri waishio Nje ya Nchi, Mhe. Dkt. Badr Abdelatty, yaliyofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini Marekani ambapo amesisitiza umuhimu wa kuongeza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo. Amesema Misri ina miradi 61 ya uwekezaji nchini Tanzania yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.5, inayotekelezwa katika sekta mbalimbali na kutoa ajira 5,364. Akizungumzia ushirikiano wa kimkakati, Waziri Kombo amesema Tanzania inathamini mchango wa kampuni za Misri katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini, hususan Mradi wa Kufua Umeme w…