TANESCO YAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO
TANESCO YAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO *Zoezi la Ukaguzi na maboresho ya miundombinu linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini Na Mwandishi Wetu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) leo Septemba 22, 206 limeendelea na kampeni yake ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya umeme salama wakati wa elnino sambamba na kueleza mikakati inayoendelea kuchukuliwa katika kuimarisha miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua za El Niño. Hatua hizo ni pamoja na kukagua miundombinu, kubaini na kutatua changamoto, pamoja na kutathmini maeneo yanayoweza kuathiriwa na mafuriko au maporomoko ya ardhi ili kuweka uthabiti wa miundombinu ya umeme. Akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja TANESCO, Bi. Irene Gowelle, amesema TANESCO imejizatiti kuhakikisha huduma ya umeme inaendelea kuwepo kwa usalama endapo mvua hizo zitanyesha. “Wananchi wanaweza kututaarifu TANESCO kama kuna …