TANESCO UBUNGO YAWANASA WEZI WA UMEME

TANESCO UBUNGO YAWANASA WEZI WA UMEME
Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ubungo jijini Dar es Salaam limeendelea na operesheni yake maalum ya kuwabaini na kuwachukulia hatua wateja ambao wanatumia umeme bila kulipia wakiwa wameunganishiwa umeme na vishoka mtaani kinyume na utaratibu. Katika operesheni hiyo TANESCO Mkoa wa Ubungo imekamata baadhi ya wateja wake katika maeneo ya Mabibo External,Mburahati na Kimara Kilungure na miongoni mwa wateja hao wamekuwa wakitumia umeme wa TANESCO bila kulipia kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Akizungumza leo Septemba 2,2026 wakati wa operesheni hiyo fundi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ubungo Salum Bure amesema wamewakamata wateja ambao wamechepusha umeme kupitia vishoka. “Katika eneo la Mtaa wa Amani uliopo Mabibo External kuna mteja tumekuta amechepusha umeme na mara ya mwisho amenunua umeme Agosti mwaka 2025.Hivyo kwa zaidi ya mwaka mmoja halipi umeme na ameunganishiwa na kishoka. “Pia katika Mtaa wa Tanzanite uliopo Kimara Kirungule kuna mteja am…