TAMISEMI YAIMARISHA MIKAKATI YA UDHIBITI WA TAKA NGUMU NA USAFI WA MAZINGIRA

TAMISEMI YAIMARISHA MIKAKATI YA UDHIBITI WA TAKA NGUMU NA USAFI WA MAZINGIRA
Na OWM-TAMISEMI, Dodoma Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) imeanza kupitia viashiria vya kupima utendaji wa Halmashauri katika usimamizi wa taka ngumu na usafi wa mazingira, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na ongezeko la taka, kulinda afya ya wananchi na kuweka mazingira ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Akifungua kikao kazi cha siku mbili leo Septemba 22, 2026, jijini Dodoma, Mratibu wa Huduma za Afya na Usafi wa Mazingira kutoka OWM-TAMISEMI, Bwana Selemani Yondu, amesema mapitio hayo yanalenga kuweka viashiria vinavyoeleweka na kupimika ili kutathmini kwa usahihi utendaji wa kila Halmashauri. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mwaka ya Utendaji wa Usimamizi wa Takangumu 2025/2026, Tanzania Bara inazalisha wastani wa tani 666,604 za taka ngumu kwa mwezi, lakini tani 368,665 pekee, sawa na asilimia 55.3, ndizo zinazokusanywa, huku tani 297,939 zikibaki bila kukusanywa. “Ingawa asilimia 97.6 ya taka zinazokusanywa hufikishwa katika maeneo yaliyotengwa k…