SUBIRA MGALU AIPA HEKO TRA BAGAMOYO KWA UBUNIFU UKUSANYAJI MAPATO
SUBIRA MGALU AIPA HEKO TRA BAGAMOYO KWA UBUNIFU UKUSANYAJI MAPATO
Na Victor Masangu, Bagamoyo MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. CPA Subira Khamisi Mgalu, ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bagamoyo kwa ubunifu na mipango madhubuti inayolenga kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato. Mhe. Mgalu aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika Ofisi za TRA Bagamoyo, ambapo alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Meneja wa TRA Bagamoyo, Mariam Omari. Katika mazungumzo hayo, walijadili masuala mbalimbali yanayohusu ongezeko la mapato, ukusanyaji wa kodi, mikakati ya kuvuka malengo ya ukusanyaji pamoja na umuhimu wa kuendelea kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuhusu ulipaji wa kodi. Mhe. Mgalu ameipongeza TRA Bagamoyo kwa kazi inayofanyika katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaendelea kuimarika, akisema hatua hizo ni muhimu katika kuchochea maendeleo ya Taifa na Jimbo la Bagamoyo. Aidha, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TRA na kuhamasisha wananchi kupitia mikutano yake mbalimbali kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa wakati il…