SERIKALI YATAKA USHAHIDI UONGOZE MAAMUZI YA MAENDELEO, WADAU WATAKA SERA YA TAIFA YA TATHMINI

SERIKALI YATAKA USHAHIDI UONGOZE MAAMUZI YA MAENDELEO, WADAU WATAKA SERA YA TAIFA YA TATHMINI
Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu wenye Ulemavu), Dk Jim Yonazi, akizungumza kwenye kongamano hilo ………. Na Happy Lazaro, Arusha. Serikali imesisitiza umuhimu wa kujenga utamaduni wa ufuatiliaji, tathmini na matumizi ya ushahidi katika kufanya maamuzi ya maendeleo nchini, ikieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kutambua changamoto mapema, kuchukua hatua kwa wakati, kujifunza kutokana na utekelezaji na kuboresha huduma kwa wananchi. Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Naibu spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Daniel Sillo kwa niaba ya Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba wakati akifungua kongamano la tano la kitaifa la wiki ya ufuatiliaji na tathmini na ujifunzaji (MEL) linaloendelea katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha . Sillo amesema kuwa ufuatiliaji na tathmini si suala la kukusanya na kuchambua takwimu pekee, bali ni chombo muhimu cha menejimenti kinachosaidia kupima utekelezaji wa malengo, kubaini changamoto na kuchukua hatua kabla hazijaathir…