SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WACHIMBAJI WADOGO LINDI
SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WACHIMBAJI WADOGO LINDI Serikali kupitia Wizara ya Madini imesema inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika kukuza uchumi wa nchi, na itaendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha kupata huduma na fursa mbalimbali zinazohitajika katika shughuli zao. Akifunga Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Lindi kwa mwaka 2026, yaliyofanyika katika Wilaya ya Ruangwa leo Septemba 19, 2026, Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Lemomo Kiruswa, amesema Wizara itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wadogo ili kuongeza uzalishaji na tija katika sekta ya madini. “Ninawaomba wachimbaji kutumia fursa zinazotolewa na Serikali na taasisi zake ili kuboresha shughuli zao na kuongeza tija katika uzalishaji,” amesema Dkt. Kiruswa. Aidha, Dkt. Kiruswa amewahimiza wachimbaji wa madini kuzingatia Sheria ya Madini, sheria za mazingira, afya na usalama mahali pa kazi, pamoja na taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali katika shughuli za uchimbaji. Ametoa wito kwa taasisi zinazohusika, ikiwemo OSHA, NE…