SAFARI YA MIAKA NANE YA MJI WA SERIKALI YAFIKIA KILELE: RAIS SAMIA KUUZINDUA SEPTEMBA 8
SAFARI YA MIAKA NANE YA MJI WA SERIKALI YAFIKIA KILELE: RAIS SAMIA KUUZINDUA SEPTEMBA 8 Na Dotto Kwilasa,Dodoma DODOMA. Safari ya takribani miaka nane ya ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma imefikia kilele, huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akitarajiwa kuuzindua rasmi Septemba 8, 2026. Uzinduzi huo utahusisha majengo ya Wizara 26, taasisi 11 za Serikali pamoja na mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilomita 57.1. Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 6, 2026 jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema kukamilika kwa Mji wa Serikali ni hatua muhimu katika utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu yenye miundombinu ya kisasa na mazingira bora ya utendaji. Amesema uzinduzi utafanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo ndani ya Mji huo. Profesa Kabudi amesema safari ya Mtumba ilianza mwaka 2018, ambapo Novemba 28, 2018 Serikali ilianza kujenga majengo 23 ya muda kwa ajili ya ofisi za Serikali. Majengo hayo yalikamilika Machi 22, 2019 na kuwezesha baadhi ya Wizara na taas…