RUWASA YAKABIDHI PIKIPIKI KUBORESHA HUDUMA ZA MAJI RUNGWE
RUWASA YAKABIDHI PIKIPIKI KUBORESHA HUDUMA ZA MAJI RUNGWE
Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imekabidhi pikipiki kwa Kamati ya Watumia Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) ya MIMAKI, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji na usimamizi wa huduma za maji kwa wananchi. Pikipiki hiyo imekabidhiwa kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi ya RUWASA na Mjumbe wa Bodi hiyo, Mhandisi Ngwisa Wilfred Mpembe, kwa chombo cha watoa huduma ya maji cha MIMAKI chenye makao makuu katika Kijiji cha Mpuguso, Kata ya Mpuguso. MIMAKI inahudumia wananchi katika vijiji 14 vilivyopo katika kata za Mpuguso, Ilima, Malindo na Kisondela, eneo ambalo lina ukubwa wa kijiografia na hivyo kuhitaji usafiri wa uhakika kwa ajili ya ufuatiliaji na utatuzi wa changamoto za huduma ya maji. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhandisi Mpembe aliwataka viongozi wa CBWSO kuhakikisha wanatumia chombo hicho kuongeza ufanisi wa huduma na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa wakati. Alisema pikipiki hiyo inapaswa …