RC SENYAMULE AIOMBA KKKT KUENDELEA KUWA NGUZO YA MAADILI, AMANI NA MAENDELEO YA TAIFA

RC SENYAMULE AIOMBA KKKT KUENDELEA KUWA NGUZO YA MAADILI, AMANI NA MAENDELEO YA TAIFA
Na Janeth Raphael - MichuziTv  Ikiwa taifa liko katika juhudi za kujenga jamii yenye maadili, amani, mshikamano na uwajibikaji, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetakiwa kuendelea kutumia nafasi yake katika kuimarisha misingi hiyo na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rose Mary Senyamule, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 6 wa Wachungaji wa KKKT unaofanyika katika Ukumbi wa Chimwaga, jijini Dodoma. Senyamule amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa KKKT katika maendeleo ya taifa, ikieleza kuwa kwa miaka mingi kanisa hilo limekuwa mshirika muhimu katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii. Amesema huduma hizo ni pamoja na elimu, afya, malezi ya vijana, huduma kwa watu wenye mahitaji maalum pamoja na misaada ya kijamii na juhudi za kupambana na umaskini.  Senyamule amesema pamoja na huduma za kijamii, KKKT imeendelea kuwa mdau katika shughuli za kiuchumi na uwekezaji, huku viongozi wa dini wakiwa na …