RAIS DKT. SAMIA KUZINDUA MIRADI KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA, DODOMA
RAIS DKT. SAMIA KUZINDUA MIRADI KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA, DODOMA
Na, Mwandishi Wetu -Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua majengo ya Ofisi za Wizara, Taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 57.1 katika Mji wa Serikali Mtumba,Jijini Dodoma. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika jumanne Septemba nane mwaka huu katika Uwanja wa Mashujaa uliopo ndani ya Mji wa Serikali Mtumba. Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma leo (06 Septemba, 2026) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Mhe.Profesa Palamagamba Kabudi, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya hafla hiyo. Alisema uzinduzi huo utahusisha maeneo matatu makuu ambayo ni majengo ya Ofisi za Wizara 26, Taasisi 11 za Serikali na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 57.1. Profesa Kabudi alisema kukamilika kwa majengo hayo, kutawezesha watumishi 18,510 kutumia ofisi za Mji wa Serikali, Mtumba. “Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba ulianza kutekelezwa kwa awamu, ambapo awa…