PSSSF YATOA ELIMU NA HUDUMA MKUTANO WA TRAMPA

PSSSF YATOA ELIMU NA HUDUMA MKUTANO WA TRAMPA
Mgeni Rasmi, Waziri Ridhiwani Kikwete, akikabidhi tuzo ya shukrani kwa PSSSF iliyopokelewa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati Bw. Sayi Lulyalya wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA). Picha ya maafisa kumbukumbu na nyaraka kutoka PSSSF, waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 14 wa TRAMPA Wanachama wa PSSSF wakihudumia kandoni mwa Mkutano Mkuu wa 14 wa Maafisa Kumbukumbu na Nyaraka kutoka Ofisi za Umma jijini Dodoma Dodoma, Septemba 23, 2026 Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeshiriki katika Mkutano wa 14 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) uliofunguliwa rasmi Jumatano, Septemba, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe, Ridhiwani Kikwete ambaye aliwataka wanachama wa TRAMPA kuhakikisha historia ya Taifa inalindwa, pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika katika ofisi za umma. Mhe. Ridhiwani Kikwete ameiagiza Taasisi…