PSSSF, TBN KUIMARISHA USHIRIKIANO UTOAJI ELIMU YA HIFADHI YA JAMII

PSSSF, TBN KUIMARISHA USHIRIKIANO UTOAJI ELIMU YA HIFADHI YA JAMII
Katika hatua inayolenga kupanua wigo wa utoaji wa elimu kwa umma, timu ya maofisa wa juu kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imefanya ziara rasmi katika Makao Makuu ya Muda ya Tanzania Bloggers Network (TBN), yaliyopo Kijitonyama, Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kimkakati na viongozi wa mtandao huo. Mazungumzo hayo yalilenga kujenga ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote mbili, hususan katika masuala ya habari, uelimishaji wa umma na usambazaji wa taarifa na maarifa sahihi kuhusu mifumo ya hifadhi ya jamii, pensheni pamoja na uwekezaji unaofanywa na PSSSF. Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa TBN, Beda Msimbe, alisema mtandao huo uko tayari kutumia majukwaa yake kusimama kidete katika kutoa elimu na kusambaza taarifa sahihi kwa umma, hususan kupitia majukwaa ya kidijitali. Hata hivyo, alisisitiza umuhimu wa wanachama wa TBN kupata mafunzo ya kina kuhusu shughuli, huduma na uendeshaji wa PSSSF, ili waweze kuwaelimisha wananchi kwa uf…