PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI (AFDP) YAWAFIKIA WAKULIMA,WAVUVI NA JAMII YA WAFUGAJI MKOANI TANGA
PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI (AFDP) YAWAFIKIA WAKULIMA,WAVUVI NA JAMII YA WAFUGAJI MKOANI TANGA
Na; Mwandishi wetu-Tanga. Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa la Kuendeleza Kilimo (IFAD) na wataalamu kutoka katika sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) wamekutana Mkoani Tanga Tarehe 7 Septemba 2026 kwa lengo la kufanya mapitio ya Utekelezaji wa Programu hiyo. Sambamba na hilo timu hiyo itatembelea maeneo yanayotekeleza Programu kwa Mkoa wa Tanga, ambapo kwa upande wa sekta ya kilimo timu hiyo itatembelea kata ya Msomela iliyopo katika Halmashauri ya Handeni Vijijini ambako programu imehamasisha na kutoa elimu ya kilimo bora kwa jamii ya kimasai ambao kiasili ni wafugaji ambapo wameweza kujishughulisha na kilimo cha mahindi chenye tija. Programu imewezesha kuwepo kwa eneo la mashamba darasa (FFS) kwa mazao ya Alizeti, Mahindi na Maharage, na shamba Darasa hilo limeonesha mafanikio kwa kiasi kikubwa, ambapo hekta moja inaweza kuzalisha takribani magunia 20 ya kilo mia moja kila moja, na jamii ya wafugaji sasa inajishulisha na shughuli za Kilimo na kunufaika na…