PROF. SHEMDOE ATOA SIKU 14 WATAALAM KUCHAMBUA HOJA ZA WANANCHI MGOGORO WA MIPAKA KAZIMZUMBWI
PROF. SHEMDOE ATOA SIKU 14 WATAALAM KUCHAMBUA HOJA ZA WANANCHI MGOGORO WA MIPAKA KAZIMZUMBWI
Na: OWM–TAMISEMI, Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, ametoa maagizo kwa Mkurugenzi anayeshughulikia Mipango Miji na Vijiji wa OWM–TAMISEMI, Kamishna wa Ardhi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara hiyo na Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kuchambua hoja zaidi ya 60 zilizowasilishwa na wananchi 22 kuhusu mgogoro wa muda mrefu wa mipaka ya kiutawala na mpaka wa Msitu wa Kazimzumbwi, ndani ya siku 14 na kuwasilisha taarifa ya uchambuzi huo. Prof. Shemdoe amesema baada ya kupokea taarifa hiyo, itawasilishwa kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ambaye atawasilisha hoja na maombi ya wananchi kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kupata maelekezo ya utatuzi wa kudumu wa mgogoro huo. Prof. Shemdoe ametoa agizo hilo Septemba 23, 2026, wakati wa mkutano na wan…