PROF. MKENDA AIBANA TCU: UDAHILI UENDANE NA UWEZO WA VYUO KULINDA UBORA WA ELIMU
PROF. MKENDA AIBANA TCU: UDAHILI UENDANE NA UWEZO WA VYUO KULINDA UBORA WA ELIMU
Na Janeth Raphael - MichuziTv WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuimarisha mfumo wa udahili na usajili wa wanafunzi wa elimu ya juu ili kuhakikisha vyuo havipokei wanafunzi zaidi ya uwezo wa miundombinu na wakufunzi waliopo. Prof. Mkenda amesema hatua hiyo ni muhimu katika kulinda ubora wa elimu ya juu nchini, huku ikihakikisha wanafunzi wanapata nafasi za masomo kwa haki, uwazi na kwa kuzingatia uwezo halisi wa kila chuo. Waziri huyo ameyasema hayo leo, Septemba 5, 2026, jijini Dodoma, baada ya kukutana na Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu pamoja na Wenyeviti wa Mabaraza ya vyuo vikuu nchini katika kikao kilichojadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya elimu ya juu, ikiwemo udahili na usajili wa wanafunzi. Amesema Serikali inalenga kuhakikisha mfumo wa udahili unakuwa bora na wenye ufanisi, ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza pale vyuo vinapodahili wanafunzi wengi kuliko uwezo wa kuwahudumia. “Tumefanya hivyo kwa…