POLISI KATA LUEGU AGEUKA DARAJA LA HURUMA KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

POLISI KATA LUEGU AGEUKA DARAJA LA HURUMA KWA WENYE MAHITAJI MAALUM
Polisi kata ya Luegu Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma CPL Mjinya Ismail akiwa katika kitongoji cha Mlambichuma akimkabidhi mzee Ally mahitaji baada ya kuwatembelea mzee huyo mwenye uhitaji pamoja na Rehema Zuberi mwenye changamoto ya akili  Polisi kata ya Luegu Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma CPL Mjinya Ismail akizungumza jambo na Rehema Zuberi ambae mwenye changamoto ya akili katika kitongoji cha Mlambichuma kilichopo kata ya Luegu wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma Na Regina Ndumbaro, Namtumbo-Ruvuma Safari ya takribani kilomita 11 kutoka Suluti stendi kuelekea Kitongoji cha Mlambichuma, kata ya Luegu Halimashauri ya wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, haikuwa safari ya kawaida kwa Polisi Kata wa Luegu, CPL Mjinya Ismail. Safari hiyo haikuhusu kufuatilia tukio la uhalifu wala operesheni ya kiusalama, bali ilikuwa safari ya kuwafikia wananchi wenye mahitaji maalum, ambao mara nyingi changamoto zao zinaweza kupita bila kuonekana na jamii. Akiwa ametoka Kituo cha Polisi Namtumbo, CPL Mjinya alif…