NGAJILO AIBANA SERIKALI KUHUSU UHAMISHWAJI WA GEREZA KUU LA IRINGA

NA DENIS MLOWE,  IRINGA  MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Fadhili Fabian Ngajilo, ameiomba Serikali kuharakisha uhamishaji wa Gereza Kuu la Iringa kutoka eneo la mjini kwenda Mlolo, Kata ya Isakalilo, ili kupisha upanuzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa. Ngajilo ametoa ombi hilo Bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayub Mohamed Mahamud, baada ya Serikali kueleza kuwa mchakato wa kuhamisha gereza hilo unaendelea . Ngajilo amesema suala la kuhamisha Gereza Kuu la Iringa limejadiliwa kwa muda mrefu, akieleza kuwa mjadala huo umeanza tangu miaka ya 1980, huku eneo la Mlolo likiwa tayari limetengwa kwa ajili ya ujenzi na uhamisho wa gereza hilo. Amesema uwepo wa gereza katika eneo la mjini umeendelea kuwa kikwazo katika upanuzi wa huduma za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, licha ya eneo hilo kuwa muhimu kwa wananchi wanaohitaji huduma za afya. Ngajilo amesema yeye kwa kushirikiana na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wame…