MWENYEKITI (UVCCM) GEITA AICHOTA TEKNOLOJIA YA MABASI KUKUZA USAFIRISHAJI CHINA

MWENYEKITI (UVCCM) GEITA AICHOTA TEKNOLOJIA YA MABASI KUKUZA USAFIRISHAJI CHINA
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita, Manjale Magambo, ametembelea kiwanda kikubwa cha kutengeneza mabasi cha Yutong kilichopo Zhengzhou nchini China kwa mwaliko rasmi. Ziara hiyo inalenga kujifunza teknolojia na mbinu za kisasa zinazotumika katika sekta ya usafirishaji ili kuona namna zinavyoweza kusaidia kukuza uchumi na kufungua fursa kwa vijana nchini. Akiwa kiwandani hapo, Magambo alipata fursa ya kujionea kwa vitendo mchakato mzima wa uzalishaji wa mabasi, kuanzia usanifu hadi hatua za mwisho, jambo lililompa uelewa wa karibu kuhusu teknolojia na mifumo bora inayotumika Akizungumza baada ya ziara hiyo, Magambo alisema China imefanikiwa kuitumia sekta ya usafirishaji kama injini muhimu ya maendeleo ya uchumi kwa kuunganisha teknolojia na ufanisi.  “Ziara hii imetupa nafasi ya kujifunza na kuona kwa vitendo namna teknolojia inavyotumika katika sekta ya usafirishaji. Tumepata uzoefu ambao tunaweza kuutumia katika kutafakari fursa mbalimbali za maen…