MWENGE WAZINDUA UPANUZI WA MFUMO WA KUSAFISHA NA KUTIBU MAJI NZEGA

MWENGE WAZINDUA UPANUZI WA MFUMO WA KUSAFISHA NA KUTIBU MAJI NZEGA
Na Mwandishi wetu, Nzega MWENGE wa uhuru kupitia kiongozi wa mbio za Mwenge 2026 Wazo Michael Mwang’onda umezindua mradi wa upanuzi wa mfumo wa kusafisha na kutibu maji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Nzega Mjini (NZUWASA). Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe Naitapwaki Tukai akizungumza September 19, mwaka 2026 mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2026 Wazo Michael Mwang’onda amesema mradi huo una manufaa makubwa kwa jamii. Mhe Naitapwaki Tukai amesema kukamilika kwa mradi huo kunasaidia uimarishaji upatikanaji wa maji na kupunguza au kuondoa magonjwa ya mlipuko yatokanayo na ukosefu wa maji. “Wananchi wa mji wa Nzega wanatumia maji kadiri wanavyohitaji kupitia miradi huu kwa kulipia kiasi wanachotaka wakitaka maji ya elfu 3 wanapata wakitaka maji ya laki moja wanapata,” amesema. Meneja wa mradi huo mhandisi Mwiyombela Humphrey akisoma taarifa ya mradi huo amesema umetekelezwa kwa muda wa miezi 36 kwa kutumia mkandarasi FABEC Investment LTD. Mhandisi Humphr…