MRADI WA “MWANAMKE NI SEHEMU YA MAAMUZI SHIRIKI NAYE ” WATAMBULISHWA SHINYANGA KUNUFAISHA WANAWAKE VIJANA

MRADI WA “MWANAMKE NI SEHEMU YA MAAMUZI SHIRIKI NAYE ” WATAMBULISHWA SHINYANGA KUNUFAISHA WANAWAKE VIJANA
Meneja miradi kutoka Shirika la Young Women Leadership Veronica Masawe akizungumza na viongozi wa Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga wakati wa kutambulisha mradi wa Mwanamke ni sehemu ya maamuzi shiriki naye utakaotekelezwa Kata ya Kizumbi na Mwawaza Na Stella Herman,Shinyanga Shirika la Young Women Leadership limetambulisha rasmi mradi wake wa “Mwanamke ni sehemu ya maamuzi shiriki naye” utakao tekelezwa katika Kata ya Kizumbi na Mwawaza Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana wanawake kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35. Akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo leo Septemba 9,2026 kwa viongozi wa Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga,Meneja miradi kutoka Shirika la Young Women Leadership Veronica Masawe,amesema mradi huo utasaidia kuwawezesha wanawake vijana kutumia fursa za maamuzi zilizopo katika maeneo yao na kushiriki fursa za kiuchumi. Amesema kupitia mradi huo utawajengea uwezo kupinga vitendo vya rushwa ya ngono,kushirika fursa za kijamii na vyombo mbalimb…