MHE. SUBIRA MGALU AIPA KONGOLE  TRA BAGAMOYO KWA JUHUDI  ZA  KUONGEZA KASI YA  UKUSANYAJI WA  MAPATO

MHE. SUBIRA MGALU AIPA KONGOLE  TRA BAGAMOYO KWA JUHUDI  ZA  KUONGEZA KASI YA  UKUSANYAJI WA  MAPATO
Na Victor Masangu,Bagamoyo  Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. CPA. Subira Khamisi Mgalu ameipongeza Mamlaka ya mapato (TRA) Bagamoyo kwa kuweka mipango madhubuti katika suala zima la  ukusanyaji wa mapato. Mhe.Subira ameyabainisha hayo  wakati alipofanya ziara yake  katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bagamoyo, ambapo amepata fursa ya kukutana   na kufanya mazungumzo na Meneja wa TRA Bagamoyo, Mariam Omari. Katika mazungumzo hayo, wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu ongezeko la mapato, ukusanyaji wa kodi, kuvuka malengo ya ukusanyaji pamoja na umuhimu wa kuendelea kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuhusu ulipaji wa kodi. Mhe. Subira Mgalu ameipongeza TRA Bagamoyo kwa kazi kubwa inayofanyika katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaendelea kuimarika.  Aidha, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kuhamasisha wananchi katika mikutano yake mbalimbali kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa na Jimbo la Bagamoyo. Mbunge huyo pia amempongeza Meneja wa TRA Bagamoyo, M…